Translation Games: Kiswahili
Dunia moja
painebook, translated by Lujayna
Mwangaza unang'ara kutoka kwa hema yangu. Ninapoinua kifunuo, ninamuona mtu mdogo mwenye rangi ya kijivu akisimama hapo.
"Mambo vipi, mwenzangu?"
"Watu wangu husafiri katika ulimwengu wakitimiza hamu za watu. Hamu yako ni nini?"
"Inaweza kuwa kitu chochote?" Kichwa changu kinaniuma kutokana na kinywaji cha tequila nilichokunywa ili kiweze kunisaidia kulala. "Vipi kuhusu amani? Dunia moja, isiyo na umaskini, utengano, siasa wala vita."
"Sawa."
Ninajipata nikiwa nimelala.
Nikiamka, kichwa changu kinaniuma huku nikifunga kambi na kuelekea kwa mlima. Hakuna trafiki. Ninawasha redio. Hakuna chochote isipokuwa sauti ya tuli.
Ninapoingia katika mtaa wangu, kila mtu ameondoka.
Bạn đang đọc truyện trên: AzTruyen.Top